Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, waungaji mkono wa Palestina katika miji ya Milan, Italia, Madrid, Uhispania, London, Uingereza, Geneva, Uswisi, Amsterdam, Uholanzi, Esche-sur-Alzette, Luxembourg, Toronto, Canada, Tokyo, Japan, na San Francisco, Marekani, wamefanya maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina na Ukanda wa Ghaza na kulaani mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo na kutoa wito wa kusitishwa mapigano katika ukanda huo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Geneva nchini Uswisi wametoa nara za ukombozi wa Palestina katika maandamano makubwa waliyofanya ya kuunga mkono Palestina na Ukanda wa Ghaza.
Waungaji mkono wa Palestina wamelaani mauaji ya waandishi wa habari ambayo hayajawahi kushuhudiwa mfano wake yaliyofanywa katika vita vya utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza, katika maandamano waliyofanya dhidi ya utawala huo haramu mjini San Francisco, Marekani, katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari Mpalestina wa televisheni ya Al Jazeera.
Waungaji mkono wa Palestina walikaa kimya kwa dakika mbili kuwakumbuka mashahidi wa Ghaza katika maandamano waliyofanya katika Mzunguko wa Dom katikati mwa Amsterdam, mji mkuu wa Uholanzi.
Jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimetonesha vikali hisia za walimwengu, ambapo katika kila pembe ya dunia watu, serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa zimekuwa zikitangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.
Katika miezi ya karibuni, waungaji mkono wa Wapalestina wamekuwa wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza kwa kufanya maandamano duniani kote.
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na nchi za Magharibi, utawala ghasibu wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji makubwa ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.../
342/